Umewahi kujiuliza kwanini wasanii wa kibongo wanapenda kujibatiza majina ya wasanii walio kiwanja..(Marekani)? Angalia majina kama P Funk, Saigon, halafu aliyeharibu zaidi ni Chid Benz kuanzia La familia, Hiyo Benz yenyewe ameifanyia Clipping toka Benzino, King Kong, Na sasa ivi The big boss. Hao ni wachache tu, sasa jiulize ghafla leo hawa jamaa mmoja wao anapata show kiwanja si unajua saivi kupiga show kiwanja si kitu cha kushangaza tena, sasa duuh! hawa jamaa watatengeneza picha ipi ya muziki wa kibongo huko watakapokuwa..? au ndo zile za Bitoz Nyangema anataka aitwe Tupac..? Kama hiyo haitoshi siku hizi wamekuja na staili ya kuchana na biti za mbele mbaya zaidi hawaangalii hata show za kufanya hivyo, kwa mfano AY kwenye show ya The Climax waliyodondoka Fat Joe na Eve alitumia biti ya Big Pimpin ya Hov kudondoka twista zake mbele ya hawa jamaa, unajua tafsiri yake ni nn? Bongo hakuna Maproducer Ndo kitu cha karibu ambacho jamaa walifiria nadhani, sasa kwa staili hii Kuna Next level kweli? Au mi ndo mtoto pori..?
Vielelezo:
Shea na Wengine
-
▶ Ijibu Hii