Bongo4ever [ B4E ]

Chat.Marafiki.Blogs.Muziki.Videos.and Fun [Yaani wewe Tu!]

Umewahi kujiuliza kwanini wasanii wa kibongo wanapenda kujibatiza majina ya wasanii walio kiwanja..(Marekani)? Angalia majina kama P Funk, Saigon, halafu aliyeharibu zaidi ni Chid Benz kuanzia La familia, Hiyo Benz yenyewe ameifanyia Clipping toka Benzino, King Kong, Na sasa ivi The big boss. Hao ni wachache tu, sasa jiulize ghafla leo hawa jamaa mmoja wao anapata show kiwanja si unajua saivi kupiga show kiwanja si kitu cha kushangaza tena, sasa duuh! hawa jamaa watatengeneza picha ipi ya muziki wa kibongo huko watakapokuwa..? au ndo zile za Bitoz Nyangema anataka aitwe Tupac..? Kama hiyo haitoshi siku hizi wamekuja na staili ya kuchana na biti za mbele mbaya zaidi hawaangalii hata show za kufanya hivyo, kwa mfano AY kwenye show ya The Climax waliyodondoka Fat Joe na Eve alitumia biti ya Big Pimpin ya Hov kudondoka twista zake mbele ya hawa jamaa, unajua tafsiri yake ni nn? Bongo hakuna Maproducer Ndo kitu cha karibu ambacho jamaa walifiria nadhani, sasa kwa staili hii Kuna Next level kweli? Au mi ndo mtoto pori..?

Shea na Wengine

Ijibu Hii

Hoja za Mjadala Huu

ukitegemea lugha ya mwingine wewe ni mtumwa wa kila jambo. tunasema kiswahili hakina maneno wakati tunakidharau, hivyo basi tutabaki am am kuvaa viatu vya marekani, kuongea kimarekani, kuvaa nguo za UK basi kila dakika tutaona waingereza ndio wenyewe duniani. hayo ni machache hivyo kwa kuwa tumekuwa watumwa wa lugha basi hata majina tunachukua ya kwao.

Ijibu Hii

RSS

Bongo4Ever-Mapenzi Kwa Nchi Ye2 Hayataishia Leo Tu,Hii Ni Forever.Alika Wabongo Unaowajua.

Yaliyojiri Punde

Masaa 22 yaliyopita
Masaa 22 yaliyopita
felister oswardy and Thomas Cassy are now friends
yesterday
Thomas Cassy added a discussion to the group RafikiChat
yo whats up aany one out there
yesterday

Makundi

© 2009   Created by B4E on Ning.   Create a Ning Network!

Beji  |  Taarifu Jambo  |  Faragha  |  Terms of Service

Sign in to chat!